Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAFANYA KIKAO CHA KWANZA NA KAMATI KUU YA KITAIFA YA MAANDALIZI YA MAONESHO YA 47 YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA (DITF 2023)

  • July 24, 2023


………………………..
03 Juni 2023.
Na. Norah Thomas-TanTrade Dar es salaam.

-----------------------
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  imekutana na kufanya kikao  cha kwanza cha kitaifa cha kamati kuu ya Maandalizi ya Maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam (DITF) 2023 yanayotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Mwl. J.K nyerere barabara ya Kilwa Dar es salaam kuanzia 28 Juni mpaka tarehe 13 Julai 2023. Kamati hii ndiyo yenye jukumu la kuratibu maandalizi ya Maonesho ya DITF kwa ujumla na inajumuisha wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

kikao hicho chenye lengo la  kujadli kwa kina mambo yatakayojiri katika kipindi cha maonesho, kimefanyika  tarehe 03 Juni 2023,  Katika ofisi za TanTrade Barabara ya Kilwa Dar es  salaam. 

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi mkuu wa TanTrade  bi. Latifa M. khamis amesema, Maonesho haya hutoa fursa  na kuwasaidia  Wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kukuza biashara zao na kuwawezeshan kutangaza na kutafuta masoko ya bidhaa na huduma wanazozalisha.

‘’ Maonesho haya husaidia kutoa fursa kwa wazalishaji wa ndani kuonesha bidhaa na huduma zao kwa lengo la kutafuta masoko na kuhamasisha uzalendo wa kupenda kutumia bidhaa za ndani, kutafuta wanunuzi wa bidhaa na huduma za ndani na nje kupitia mikutano ya Ana kwa Ana ya  Wafanyabiashara(B2B)  na  Buyer Seller Meetings pia Maonesho haya husaidia kuwaunganisha wazalisha wa ndani wa mazao na bidhaa na wazalishaji wa teknolojia za kisasa kutoka ndani na nje ya nchi  na kuiwezesha Serikali kupata mapato kupitia ada za ushiriki, viingilio, udhamini na michango mbalimbali’’ alisema.

Aidha bi. Latifa aliongeza kuwa, Kauli mbiu ya Maonesho 47 ya DITF 2023 ni ‘Tanzania: Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji’ (Tanzania :your Best Destination for Business and Investment)

‘’kauli mbiu hii imechaguliwa kutumika katika maonesho haya kwa ajili ya kuonesha kwamba Tanzania ni  sehemu sahihi ya kufanya biashara ambapo kuna mazingira thabiti ya biashara, utulivu na yanayofaa kwa ukuaji wa biashara na uwekezaji., hivyo kauli mbiu hii inahamasisha washiriki kutumia jukwaa hili la Maonesho ya DITF ili kupata  kupata fursa za kutangaza bidhaa na huduma zao na udhamini na michango mbalimbali’’. Alisisitiza.

Pia  Mwenyekiti wa Kamati ya  Maandalizi ambae pia ni Afisa Biashara wa Mkoa wa Dar es salaam,  Bw.  Thabit Massa ameongeza kuwa TanTrade kwa kushirikiana na DART wataanzisha njia mpya ya usafirishaji kwa Washiriki na Watembeleaji  wa Maonesho hayo, usafiri huo utaanza kutokea DART  Gerezani na Mbagala kuelekea viwanja  vya maonesho (Saba Saba).