Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAMHURI YA CZECH NCHINI

  • October 3, 2023

3 Oktoba, 2023
DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bw. Fortunatus Mhambe alipata wasaa wa kuzungumza na Mhe.  Ing. Roman Grolig, Kanseli Mkuu wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania alipokuwa anakagua maandalizi ya ushiriki wa Kampuni ya Airplanes Afrika Limited (AAL) ya nchini Czech kwenye Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Viwanda Tanzania.

Kampuni ya AAL imewekeza kwa kuanzisha kiwanda cha kwanza nchini cha kutengeneza ndege kilichopo Morogoro. Uwekezaji huo wa zaidi Ya Dola za Kimarekani milioni 7 unafanyika katika Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Jemedari Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine waliongelea kuhusu hali ya uwekezaji nchini ambapo kiwanda hicho kinampango wa kuwekeza katika maeneo mengine matano ikiwamo kiwanda cha kutengeneza betri za magari.

Bw. Mhambe alipongeza juhudi zinazochukuliwa na Ubalozi huo katika kuhamasisha kampuni za Czech kuja kuwekeza nchini na kuwaahidi kuwa Serikali ipo kwa ajili ya wawekezaji na itawasaidia sehemu yoyote itakayokuwa na changamoto katika uwekezaji wao ili kuvutia kampuni nyingi zaidi za nchi hiyo kuja kuwekeza nchini.

Pia, Bw. Mhambe alipongeza ushiriki wa kampuni hiyo katika Maonesho hayo wakiwa na bidhaa ya kipekee.