TANTRADE YARUDISHA KWA JAMII KUPITIA WATOTO AFRIKA
- September 16, 2025
15 SEPTEMBA, 2025.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade ) katika kutekeleza majukumu yake ya kurudisha kwa jamii (CSR), imeendelea kuwa taa ya matumaini kwa jamii zenye mahitaji ambapo
imefanyika faraja katika kituo cha kulelea Watoto Yatima kinachoitwa Watoto Afrika, kilichopo Jijini Mwanza. Hatua hii, imelenga kuimarisha upendo, mshikamano na kuendeleza ustawi wa jamii, katika kuchochea maendeleo jumuishi kupitia mchango wake wa kijamii na kiuchumi.