Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2025

Kura yako haki yako, jitokeze kupiga kura

Uchaguzi 2025

TANTRADE YAPATIWA MAFUNZO YA KIITIFAKI.

  • October 3, 2025

2 OKTOBA, 2025.


Watumishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) wapatiwa mafunzo ya kiitifaki ili yawaongoze vyema kwenye utendaji wa ndani ya Tanzania pamoja na ule wa Kimataifa. Mafunzo hayo yameangazia namna ya itifaki kwenye upande kibiashara kwa kuzingatia sera, utamaduni wa nchi husika, maeneo yaliyo pewa kipaumbele ni mpangili wa kuketi wa kiitifaki, vyeo, umakini kwenye kuandika na kutaja majina ya viongozi, namna ya kupokea ujumbe, kutunza muda, kuzingatia mavazi rasmi, urasimu wa mawasiliano, taarifa kabla tukio, agenda za mikutano na vikao, umakini katika mawasiliano ya simu, miongozo ya kutoa na kupokea zawadi mbalimbali kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma nk. Mafunzo ya itifaki yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kilimanjaro uliopo katika Ofisi za TanTrade zilizopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.