TANTRADE YAPATA MAFUNZO KUHUSU MUUNDO WA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI
- February 4, 2025

Watumishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bi Latifa M. Khamis, wamepata mafunzo maalum ya muundo wa ushirikiano kati ya sekta ya Umma na sekta Binafsi (PPP) , yaliyofanyika leo tarehe 3 Februari, 2025 katika Ofisi za TanTrade zilizopo katika Uwanja wa Mwl. JK Nyerere, barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Aidha mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo watumishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade )ili kuendana na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050,kwa kuingia ubia na sekta Binafsi ili kukuza uchumi wa Taasisi na Taifa kwa ujumla.