Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WATUMISHI WANAWAKE WA TANTRADE WATOA MSAADA WA VITI VYA WAGONJWA

  • June 13, 2024

13/06/2024
Dar es salaam

Watumishi wanawake wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) wametoa msaada wa viti vitatu vya wagonjwa (Wheel Chair) katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Temeke leo jijini Dar es salaam.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi Mary Fedelis ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za uendeshaji TanTrade amesema kuwa wametoa msaada huo wa viti vya wagongwa ikiwa ni kuonesha upendo kwa watu wenye uhitaji wa viti hivyo.

Aidha kwa upande wake Dkt Husna Msangi ambaye ni Daktari bingwa wa Macho katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Temeke amepokea msaada huo kwa niaba ya Mgaga Mfawidhi wa Hospitali hiyo amewashukuru watumishi wanawake wa TanTrade kwa kuunga mkono utoaji wa huduma za afya na kusema kuwa viti hivyo vitatumika katika kuboresha utoaji huduma katika hospitali hiyo.