TANTRADE YAWEZESHA WAFANYABIASHARA KUKAMATA FURSA NCHINI KOMORO
- August 23, 2024

Moroni, Komoro
21 Agosti, 2024.
Wafanyabiashara wa Tanzania wamepata fursa ya kushiriki katika kongamano la Biashara na Uwekezaji ambapo kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Komoro kwa kushirikiana na TanTrade na Kituo cha Uwekezaji Tanzania ambalo limefanyika nchini Komoro katika Ukumbi wa Bunge Moroni na kuwezesha wafanyabiashara zaidi ya 50 kutoka nchini kushiriki.
Aidha wafanyabiashara walioshiriki ni wadau katika sekta za kilimo, ufugaji na usafirishaji ambapo Taasisi za Umma na binafsi zimeshiriki ikiwa ni pamoja na Shirima la ndege ya Tanzania- Air Tanzania na PrecionAir, Mamlaka ya Bandari, Ofisi ya Mkoa wa Mtwara na Benki ya Exim.
Akizungumza katika Kongamano hilo Gavana wa jimbo la Ngazija Mtukufu Ibarahim Mzee ambaye ni Mgeni Rasmi amesisitiza uaminifu katika Biashara na Uwekezaji kwa pande zote ili kupata manufaa hasa ukizingatiwa umuhimu wa Biashara kati ya Kariakoo na Moroni.
Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Said Yakub ametoa rai kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa na Ubalozi utaendelea kushirikiana kikamilifu na TanTrade na TIC kuhakikisha wanafanikiwa katika Biashara na Uwekezaji pande zote