Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WATUMISHI TANTRADE WATAKIWA KUENDELEA KUITUMIKIA SERIKALI KWA USHIRIKIANO NA WELEDI HALI YA JUU

  • June 6, 2023

24 Mei, 2023

Na. N. Thomas - TanTrade Dar es Salaam

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis wakati wa hafla ya kuwaaga Watumishi waliostaafu na kuwapongeza Watumishi Waliofanya vizuri kwa mwaka 2022/2023 iliyofanyika katika Uwanja wa Mwl. J.K Nyerere barabara ya Kilwa, Dar es salaam.

Akiongea katika hafla hiyo Bi. Latifa
amewapongeza Watumishi hao kwa kumaliza muda wao wa Utumishi salama na kuwapongeza kwa kazi nzuri walioifanya katika kuwahudumia Wafanyabiashara.

Pia alieleza dhamira ya Serikali ya Tanzania ni kuchochea na kuendeleza uhusiano wa karibu baina ya Serikali na Wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi ili kuinua uchumi wa nchi, ivyo ametoa rai kwa Watumishi wa TanTrade kutumia nguvu na uwezo wa utendaji wa kazi waliopewa na Mwenyezi Mungu kwa ubunifu na uaminifu katika kuwahudumia wafanyabiashara kwa weredi wa hali ya juu ili kufikia dhamira hiyo kwa viwango vya juu.

"Kukiwa na ubunifu na Huduma Bora katika utendaji kazi tutaendelea kutatua kero na changamoto za kibiashara na kusapoti jitihada anazozifanya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu ya kuendelea kuifanya Tanzania kuwa mahali sahihi na salama kwa biashara na kuvutia Uwekezaji".

Pia aliongeza kuwa,
Ili kuweza kutekeleza kikamilifu vipaumbele hivyo, mchango wa wadau wa sekta ya biashara ni muhimu zaidi ili kuboresha ubora wa huduma zitolewazo na watoa huduma wa TanTrade.

"Tunapoelekea ukingoni katika maandalizi ya Maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba, tunahitaji kuunganisha nguvu za pamoja na kuendelea kujituma na kutoa huduma bora kwa Wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi ili kuwa na ufanisi wa kazi pamoja na kuimarisha uratibu na kuvutia Maonesho, ni muhimu kuzingatia mchango na mawazo ya wadau wetu".

Kwa upande wake Bi. Magreth Kiama akizungumza kwa niaba ya Watumishi waliostaafu ameishukuru Serikali ya Tanzania chini ya Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara na Watumishi wa TanTrade kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wa kipindi chake cha Utumishi.

"Nitoe Shukrani zangu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuamini na kutupatia nafasi ya utumishi kwa kipindi tulichohudumu katika wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara ivyo
napenda kutoa wito kwa Watumishi wote waliobaki kuendelea kufanya kazi kwa umoja, upendo na Ushirikiano ili kuendelea kuboresha mazingira mazuri ya wafanyabiashara na hatimaye kuimarisha uchumi na kujenga Tanzania yenye maendeleo endelevu.