Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WATUMISHI WA TANTRADE WAPATA SEMINA YA MAHITAJI YA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA

  • May 14, 2024

Dar es salaam,
Tarehe 13 Mei 2024

Mkurugezi Mkuu wa  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade Bi Latifa M Khamis siku ya leo amefungua mafunzo kwa watumishi wa TanTrade ambayo yalikuwa yanalenga kutoa elimu kwa watumishi hao juu ya namna bora ya kuandaa mahitaji ya Mafunzo kwa watumishi wa Umma.

Mafunzo hayo yametolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yamelenga kuelimisha watumishi wa umma jinsi ya kutathmini mahitaji ya mafunzo kwa Mtumishi ili kumuongezea utaalam katika fani yake na kumuwezesha kupanda ngazi katika utumishi wake wa umma.