TANTRADE YAFANYA ZIARA YA UTALII WA NDANI MKOANI GEITA
- September 29, 2023

Tarehe 27/9/2023
TanTrade ambao ni Waratibu wa Maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini wakishirikiana na Ofisi ya Jiji la Geita na Mkoa wa Geita wamefanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya Utalii na Uwekezaji Mjini Geita ili kuona fursa zilizopo mkoani Geita.
Msafara wa Ziara hiyo ulikuwa na Washiriki kutoka nchi ya Uganda, Burundi, Kenya, Taasisi za Serikali na Binafsi na walitembelea Kisiwa cha Rubondo, GGML & Underground na Buckreef.
Wadau walifurahishwa na Utalii wa ndani na kuwashukuru waratibu kwa kupata uelewa katika tasinia ya mnyororo wa thamani wa Madini.
Aidha washiriki wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshiwa Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuwaendeleza wachimbaji wadogo na wakubwa wa Madini nchini.