Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAJADILI UKUZAJI BIASHARA KATI YA TANZANIA NA UINGEREZA

  • February 1, 2024

Dar es salaam,
01 Februari, 2024

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade) imefanya mazungumzo na Kampuni ya FREMU yenye makao makuu nchini UINGEREZA ambayo hujishughulisha na  Ukuzaji wa Bidhaa za Vyakula kutoka Afrika kwenda Uingereza. lengo la mazungumzo haya ni kutathmini namna ya kushirikisha Watanzania hususan kwa bidhaa zitokanazo  na mazao  zenye mahitaji makubwa.

Akizungumza katika kikao hicho mtendaji Mkuu wa FREMU bw. David Musika ameelezea kuwa na zaidi ya Maduka 500 nchini humo pamoja na Supermarkets zinazouza bidhaa za Kilimo kutoka Afrika ambazo huwezesha Jamii zenye kupendelea vyakula vya tamaduni za Kiafrika kupata mahitaji hayo.Ili Tanzania inufaike zaidi imeshauriwa kurajimu( brand) bidhaa zake ili kuwa na Masoko na mikataba endelevu. Aidha, Mkuu huyo amebainisha kuwa baadhi ya bidhaa hizo ni pamoja na jamii ya kunde, unga maalum wa mhogo, viungo na Mboga hususan zilizosindikwa na kuonesha sampuli za ufungashaji zinazokubalika.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis alieambatana na Wataalam wake, ameipongeza kampuni ya FREMU na ujumbe wake kwa  kuleta taarifa  husika  na kusisiyiza kampuni ya hiyo kuendelea kutoa ushirikiano zaidi wakati wataalam wanaendelea kufanya uchambuzi wa kina kibiashara ili kuunganisha makampuni ya Tanzania na fursa hizo.

Kwa kuwa baadhi ya mahitaji yatategemea hali za uzalishaji na ugavi, miundombinu ya uhifadhi na usafirishaji na mitaji, Watendaji wote wawili wamekubaliana kushirikisha Mamlaka zingine na kufanya kazi kwa kushirikiana kimifumo ili kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Uingereza.

Kwa taarifa za kibiashara na taratibu za mauzo nje tembelea:
#Instagram: tantradetz
#Trade Portal: https://trade.tanzania.go.tz/