Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YARATIBU MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA WANAWAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM

  • May 9, 2024

09/05/2024
Dar es salaam


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa biashara Wanawake Wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es salaam leo katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.


Mgeni rasmi katika mafunzo hayo ni Bw. Crispin Luanda aliyemwakilisha Mkurungenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa M Khamis ambapo katika hotuba yake iliyowasilishwa na Bw Chrispin amewapongeza wanawake hao kwa kuzidi kuendelea kupambana katika shughuli za Biashara na Uchumi na kusema kuwa anatamani siku moja kuwaona wanawake hao katika nafasi za juu za maendeleo.
 

Bw Luanda ametoa rai kwa Maafisa Biashara wanawake kushirikiana na Maafisa wa TanTrade kuimarisha mifumo mbalimbali iliyobuniwa na Taasisi kwa kuingiza taarifa husika za bei za bidhaa katika Masoko kwani upatikanaji wa taarifa hizo utawasaidia kuimarisha biashara zao


TanTrade pia imetoa mafunzo ya mifumo ya Tantrade Biashara App pamoja na Tantrade Portal ambayo itakuwa  chachu kwa wafanyabiashara hao katika kufahamu  taarifa mbalimbali za biashara ikiwemo Masoko na Bidhaa kwa ujumla.


Mwisho Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu katika Mafunzo hayo alitumia jukwaa hilo kwa kuwaalika wafanyabiashara walijitokeza katika mafunzo hayo kuweza kushiriki Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam tayakayoanza June 28 hadi Julai 13, 2024