TANTRADE YARATIBU KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA KOREA KUSINI
- May 10, 2024

10 Mei 2024
Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis na Mtendaji Mkuu wa KOIMA Mr. leo wameongoza kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Korea Kusini ambalo linalenga kuunganisha wafanyabiashara katika sekta ya Kilimo, Usafirishaji, Nguo na Madini.
Kongamano hili limeonesha fursa mbalimbali za biashara ambazo ziko katika Sekta tajwa na jinsi ambavyo wafanyabiashara wa Kitanzania watafaidika na fursa hizo za kuuza bidhaa nchini Korea Kusini.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa amewaomba wadau katika sekta tajwa kuchangamkia fursa ya kuuza bidhaa kama Kahawa, Chai, matunda yaliyokaushwa, Madini ya Nikel, Dhahabu na Chrome, pamoja na bidhaa za nguo ambazo zina uhitaji mkubwa nchini Korea Kusini.
Pia alichukua nafasi hiyo kuwaribisha wadau wa South Korea na wadau wa ndani katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam yatakayoanza tar 28 Juni hadi 13 Julai 2024 katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaa