Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YARATIBU KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MISRI

  • January 30, 2024

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Misri, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Imeratibu Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya wafanyabiashara wa Misri na Tanzania ambapo Wadau kutoka Sekta mbalimbali likiwemo dawa, Vifaa Tiba na vipodozi, usindikaji, Ujenzi na Utalii wameshiriki.  

Mgeni rasmi alikuwa Amr Selim, Naibu Balozi, Ubalozi wa Misri nchini Tanzania. Aidha, Bw. Haroun Rashid   alimwakilisha Balozi wa Tanzania nchini Misri.
Akimwakilisha Mkurugenzi wa TanTrade, Bw. Mohamed Tajiri ( Meneja wa Ukuzaji Biashara) ametoa rai kwa Wafanyabiashara wa pande zote  kuzingatia mikataba ya kibiashara watakayokubaliana  ili kuwa na matokeo mazuri yenye tija.