Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YACHANGIA UPATIKANAJI WA MKATABA WA MAHUSIANO (MOU) KATI YA TANZANIA BAKERS ASSOCIATION NA(TBA )NA PUM NETHERLAND.

  • July 21, 2023

.......................

Na. Norah Thomas- TanTrade Dar es salaam.
27 APRIL,2023.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki kikamilifu na kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano ya kibiashara na uwekezaji  kati ya Chama Cha Uokaji Tanzania (TBA) na kampuni kutoka uholanzi (PUM Netherland) uliofanyika katika Ubalozi wa Uholanzi jijini Dar es salaam.

 akizungumza katika kongamano hilo Mwenyekiti wa TBA  Bi. Fransisca Lyimo amesema, kwa sasa wanaanza kutoa elimu ya uokaji kwa watu wote, baadae wataingia mpaka mashuleni kuwapatia Wanafunzi elimu hii itakayowasaidia kuwajenga kiakili na kimaarifa, na pia elimu hii itasaidia kuleta ajira kwa vijana wengi, ivyo natoa wito kwa Watanzania kuangalia fursa zilizopo katika Tasnia hii ya uokaji.

Pia, Afisa biashara kutoka TanTrade bwana Fredy Liundi akimuakilisha Mkurugenzi Mkuu bi. Latifa Khamis amesema kuwa, ikiwa ni moja kati ya shughuli za TanTrade ambazo ni kusaidia Wajasiliamali na Wafanyabiashara katika kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi, ivyo TanTrade imefanya kazi kwa ukaribu sana na TBA na kuwaunganisha na Wajasiliamali mbalimbali, na kuwapatia mafunzo ya uokaji ambayo yamewasaidia katika shughuli za ukuzaji uchumi binafsi na nchi kwa ujumla, hivyo Mkataba huu utasaidia sana kuinua sekta ya Uokaji na kuchochoa uchumi wa Tanzania.

‘’Serikali ya Tanzania, inatambua mchango mkubwa wa sekta ya uokaji katika kuzalisha ajira na kuchochea uchumi, hivyo hatuna budi kuwaunga mkono na kuwapa nguvu waokaji wa Tanzania ili kuhakikisha kuwa sekta ya uokaji inaendelea kukua na kupata mafanikio’’ alisema Bw. Liundi.