TANTRADE INAENDELEA KUWAHUDUMIA WAFANYABIASHARA SEKTA YA KILIMO KWENYE MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO NANENANE 2025.
- August 8, 2025
7 AGOSTI, 2025
NZUGUNI, DODOMA.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inaendelea kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara kutoka sekta ya Kilimo kwa kuwapatia elimu ya biashara, matumizi ya teknolojia kwenye biashara kwa kutumia mifumo mbalimbali inayoratibiwa na TanTrade kama vile Trade Portal, Biashara App. Wafanyabiashara hao wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwenye Banda la TanTrade kwaajili ya kutambua fursa mbalimbali zinazopatikana endapo watumia chapa ya Made in Tanzania kwenye bidhaa na huduma wanazozizalisha. Maonesho ya Nanenane kwa mwaka 2025, yamebeba kauli mbiu inayosema "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo". Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yameanza tarehe 1 Agosti na yatatamatika tarehe 8 Agosti 2025 Jijini Dodoma.