Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAENDELEA KUTOA HUDUMA KABAMBE KWA WAFANYABIASHARA WA SEKTA YA NISHATI

  • November 12, 2024

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade imeendelea kutoa suluhisho kwa wafanya Biashara na Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa kutoa huduma  mbalimbali kupitia banda lake lililopo katika Kongamano la Uwekezajı katika sekta ya Nishati.
Aidha TanTrade inatoa vibali na kusimamia Matukio ya Ukuzaji Biashara (Trade promotion events)yanayofanyika nchini  Kwa lengo la kuimarisha sekta ya Biashara ili kuleta matokeo chanya kwenye ukuaji wa Uchumi nchini Tanzania

Kongamano hilo limelenga kuchechemua fursa zinazohusu Uwekezajı katika sekta ya Nishati nchini, wadau mbalimbali wa Nishati wameshiriki kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano katika Hoteli ya Johari Rotana, kongamano hili limeratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na kuandaliwa na  HBZ pamoja na TAOMAC Dar es Salaam, Leo tarehe 12, Novemba 2024.