Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAENDELEA KUWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA KUTUMIA FURSA ZA SOKO HURU LA AFRIKA

  • September 3, 2023

NJOMBE
01 Septemba, 2023.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) , imeendelea kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa mkoa wa Njombe juu ya kutumia fursa za kibiashara kwenye soko huru la Afrika (AfCFTA).
Mkoa wa Njombe ni Kati ya maeneo yanayozalisha  mazao mbalimbali kwa wingi ikiwemo Parachichi, viazi mviringo na mazao  yanayotokana na miti.
Katika kikao cha kuwajengea ufahamu juu ya soko huru la Afrika wafanyabiashara wamefahamishwa juu ya fursa zilizopo katika eneo huru la kibiashara Afrika, vikwazo vya kibiashara vilivyopo na namna ya kukabiliana navyo pamoja na kutumia mifumo ya kidijitali katika kufanya biashara zao.
Wafanyabiashara wa mkoa wa Njombe wameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia  TanTrade kwa kuwafikia na kuwapa elimu juu ya Soko Huru la Afrika na wametoa wito kwa mamlaka zilizo ngazi ya wilaya na Halmashauri kuwa wapesi katika kuwatatulia changamoto zao pindi wanapoziwasilisha.
Wafanyabiashara hao wameibua changamoto mbalimbali zinazowafanya kushindwa kulifikia soko la Afrika zikiwemo; elimu juu ya vifungashio vyenye ubora na viwango vinavyokubalika kwenye biashara ya kimataifa, urasimu wa kupatiwa vibali  na mitaji yao kuwa midogo.
Aidha wameiomba Serikali kuongeza kasi ya kuvutia wawekezaji mkoani Njombe ili kuwawezesha kupata mahitaji ya kibiashara kama vile vifungashio kwa karibu ili kupunguza gharama katika biashara zao.
Aidha, Wafanyabiashara wa Mkoa wa Njombe wameonesha utayari wa kufanya biashara katika Soko Huru la Afrika