Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAENDELEA KUPIGA CHAPUO KWA WAZALISHAJI WA TANZANIA KUINGIA MASOKO YA KIMATAIFA KUPITIA MIKUTANO YA AGRF 2023

  • September 7, 2023

_________________
DAR ES SALAAM,
07 SEPTEMBA, 2023

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) imeendelea kupaisha  makampuni ya Tanzania kupitia Maonesho yanayokwenda sambamba na program za Mikutano ya Mifumo ya usalama wa Chakula Afrika (AGRF2023) inayoendelea katika kituo cha JNICC Dar es salaam hadi tarehe 8 Septemba 2023.

 Kampuni hizo zimepatiwa eneo maalum  la Bazaar kupitia mwavuli wa TanTrade ambapo wanaonesha bidhaa za kimkakati zilizozalishwa na kufungashwa kukidhi viwango vya kimataifa ikiwemo Korosho, kahawa, chai, nafaka, kokoa na nyinginezo.Lengo Kuu ni kufungua masoko kwa kuhamasisha mauzo ya nje (exports) ili kuchagiza mapato ya fedha za kigeni,  ajira na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Awali, miongoni mwa wadau muhimu na Viongozi mbalimbali waliotembelea ni pamoja na
Mhe Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye  alipongeza juhudi  za kutangaza bidhaa za nchi na pia kutoa maoni kuwa  Maonesho makubwa ya viwanda yanayotarajiwa Oktoba 2023 ya TIMEXPO  yanayoandaliwa na TanTrade na CTI mialiko  iwafikie  wadau wa Njombe pia waweze kushiriki kikamilifu kwa kuwa ni fursa za kuonesha wanachozalisha, kuonana na wanunuzi watarajiwa na vile vile kuzitambulisha bidhaa mpya sokoni.