Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAKUTANISHA KAMPUNI ZA TANZANIA NA DUBUY.COM

  • July 18, 2024

Dar es Salaam.
Tarehe 18 Julai, 2024.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu kikao cha Biashara kati ya kampuni za Tanzania na DUBUY.COM kampuni tanzu ya DP World.

Kikao hicho kimelenga kurahisisha biashara ya Kimataifa (Exports & Imports) ya kampuni za ndani kupitia huduma za Dubuy.Com kwa kuratibu ununuzi na Usafirishaji wa mali ghafi kwa gharama nafuu na kuwahakikishia soko la kimataifa na malipo kwa kampuni zinapouza bidhaa nje ya nchi.

Akifungua kikao hicho, Bi. Latifa M. Khamis, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade alieleza kuwa Mamlaka inajukumu la kuunganisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana fursa zinazoongeza ufanisi katika uzalishaji na biashara.

Alimalizia kwa kusisitiza kuwa kikao hiki kitafungua milango kwa Wadau wa Biashara toka Tanzania kufanya biashara kubwa zaidi nje ya mipaka ya Tanzania.