Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAKUTANISHA WADAU WA SEKTA YA NISHATI NA MADINI TANZANIA NA IRAN

  • February 23, 2024

Dar es Salaam.
21 Februari 2024

TanTrade imeratibu mkutano wa Kibiashara (B2B) kati ya wadau wa Sekta ya Madini na Nishati wa Tanzania na Iran wenye lengo la kujadili ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika kuendeleza mashirikiano ya kibiashara.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya Madini na Nishati kililenga kujadili fursa za Biashara na Uwekezaji katika sekta hizo muhimu kiuchumi.

Kwa upande wa nishati, Mhe. Balozi Hussein Alvandi Behineh, Balozi wa Iran nchini Tanzania na wawakilishi kutoka Iran walikutana na wataalamu wa Tanzania na kuazimia kusaini makubaliano ya ushirikiano katika kukuza biashara kati ya nchi hizi mbili.

 Katika Sekta ya Madini Kampuni ya Iran imeunganishwa na Kampuni za Tanzania kwa ajili ya kununua madini wakati wakijipanga kwa ajili ya Uwekezaji na kupata taarifa za miradi.

TanTrade inawakaribisha Jumuiya ya Wafanyabiashara kuendelea kushiriki fursa mbalimbali zinazotangazwa mara kwa mara Ili kukuza Biashara zao Kimataifa