Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAKUTANISHA TAASISI ZA UMMA NA UJUMBE TOKA IRAN

  • May 15, 2024

15 Mei 2024,
Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis leo amepokea  ujumbe kutoka Iran ambao umeongozwa na Mhe.Meisam Abedi ambaye ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Iran.

Ujumbe huu umelenga katika kuangazia fursa za Mawasiliano na Teknolojia ambazo zinapatikana Iran kwa faida ya Taasisi za serikali zenye majukumu katika eneo la Usalama wa Anga la Mtandao, Huduma za Dijitali, Usalama wa mifumo ya Serikali na Teknolojia ya Faiba na FTTH.

Katika mazungumzo yao Bi. Latifa ameelezea jinsi ambavyo TanTrade imekuwa ikishirikiana na Iran kupitia Serikali, Taasisi zake na Kampuni mbalimbali ambazo zinafanya biashara Tanzania kutoka Iran, na kumekuwa na mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali ambayo wamefanya mashirikiano.

Aidha Mhe. Meisam Abedi  ameishukuru TanTrade na kuongeza kuwa Iran iko tayari kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha wanabadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo kwenye eneo la Akili Mnemba, fire Wall, Black chain, Crypto currency na Cyber Security.