Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAWAKUTANISHA WAKULIMA WA ZABIBU NA TAASISI WEZESHI KATIKA KUONGEZA THAMANI YA ZAO LA ZABIBU

  • April 13, 2024

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  kupitia Ofisi ya Jijini Dodoma imeendelea kutoa elimu kwa wakulima wa Zabibu mkoani humo ambapo zaidi ya wakulima 100 wamepata elimu ya teknolojia rahisi ya usindikaji wa zao la Zabibu.

 
Elimu hiyo imetolewa na ofisi ya kanda TanTrade Dodoma wakati wa mkutano wa kuwaunganisha wakulima wa Zabibu na Taasisi wezeshi ili kukuza mnyororo  wa thamani.