Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE KUWAUNGANISHA WADAU WA HUDUMA ZA AFYA

  • August 6, 2024

Dar Es Salaam
5 Agosti, 2024.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi Latifa M. Khamis amekutana na Bi Negin Affarar ambaye ni muwakilishi kutoka Acibadem Group of Hospital ya Uturuki, alipofanya ziara iliyo lenga kuboresha upatikanaji wa huduma katika sekta ya  Afya wakati alipotembelea ofisi za TanTrade zilizopo katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl.  J.K Nyerere,  barabara ya kilwa jijini Dar es salaam.

Aidha, Bi Latifa alibainisha kuwa TanTrade itawaunganisha na sekta husika ili wapate kubadilishana uwezo  na kufanikisha azma yao ya utoaji wa huduma bora kwa gharama nafuu.

Bi. Negin amebainisha kuwa  Hospitali ya Acibadem Group ya Uturuki watatoa huduma katika sekta ya afya wakilenga kupunguza gharama za vipimo, matibabu, bima za afya, na kusafirisha wagonjwa kwenda kutibiwa nchini  Uturuki.