Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE NA UCSAF WAINGIA MKATABA WA KUBORESHA TEKNOLOJIA ZA MAWASILIANO (INTERNET-Wifi) KATIKA UWANJA WA MAONESHO YA SABASABA.

  • June 13, 2023



Na. Norah Thomas--TanTrade, Dar es salaam.

-----------------

08 Juni,2023.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na Taasisi ya UCSAF  wamekutana na kufanya kikao cha Makubaliano ya kuweka WiFi (Wireless Internet) kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K Nyerere kwa kipindi chote cha  Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (almaarufu Maonesho ya SabaSaba) yatakayofanyika kuanzia tarehe 28 Juni - 13 Julai, 2023. 

Kikao hicho chenye  kimefanyika  leo  tarehe 08 Juni 2023,  katika Ofisi za TanTrade Dar es Salaaam kwa lengo la  kuboresha na kurahisisha miundombinu ya nyanja ya  mawasiliano ili  kuwasaidia Washiriki pamoja na Watembeleaji kuweza kupata Mawasiliano kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi  katika kipindi chote cha Maonesho hayo.

Akizungumza katika kikao hicho, Bw. Fortunatus Mhambe, Kaimu Mkurugenzi wa Ukuzaji wa  Biashara TanTrade kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bi. Latifa M. Khamis  ameishukuru  kampuni ya UCSAF kwa kutoa huduma hiyo inayolenga kurahisisha mawasiliano na kuboresha Maonesho  yawe na mvuto zaidi.

‘Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, natoa shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya UCSAF kwa  kukubali kuboresha huduma za internet katika kipindi cha Maonesho, hivyo tunapenda kuuhabarisha Umma kwamba katika Maonesho hayo, huduma za Internet zitakuwa zimeimarishwa na kuboreshwa kwa ajili ya Watembeleaji na Waoneshaji na kuwarahisishia kuonesha biashara zao kwa njia rahisi zaidi’ Alisema.

Naye Mratibu kutoka UCSAF - Kanda ya Pwani Bw. Baraka Elieza amesema kuwa Kampuni ya UCSAF itahakikisha kuwa huduma za Internet zinakuwa nzuri na zenye kuleta tija katika Uwanja wa Maonesho na kuwafanya Waoneshaji pamoja Watembeleaji kuweza kufurahia huduma hizo. ate: 28 th june to 13th july, 2023