Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE NA UBALOZI WA MISRI KUAANDA MIKUTANO YA B2B KATIKA SEKTA YA HOTELI NA VIFAA VYA NYUMBANI

  • July 24, 2023


.................................
Na. Norah Thomas-TanTrade 
20 Juni 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis @latifa_khamis01 leo tarehe 20 Juni, 2023 katika ofisi za TanTrade amekutana na Maafisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Ukiongozwa na Ndugu Mohammad Ally Atteya na Bi. Leila Adel, ambapo wamezungumzia maandalizi ya Maonesho na Mikutano ya B2B katika sekta ya Hoteli na Vifaa vya nyumbani kutoka Misri.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 17-19 Julai, 2023, Zanzibar ambapo Kampuni takriban 15 za Misri kwenye Sekta ya Utalii zitashiriki.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis amesema TanTrade itashirikiana na Ubalozi wa Misri katika uratibu kwa kutoa wataalam kutoka TanTrade Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo.

Katika Mkutano huo kutakuwa na Maonesho madogo ya Bidhaa pamoja na mikutano baina ya wafanyabiashara (B2B) wa Tanzania Misri.

Pamoja na kuwahakikishia ushirikiano, Mkurugenzi Mkuu aliwakaribisha kutembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 Juni -13 July, 2023 katika Uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere.