TANTRADE NA UBALOZI WA CHINA WAFANYA KIKAO KAZI KUKUZA BIASHARA
- June 18, 2024

Dar es Salaam
17 Juni 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania( TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis ameushukuru Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha inaunganisha Tanzania na China katika Nyanja mbalimbali za fursa za kibiashara wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ofisi TanTrade jiji Dar es Salaam.
Bi. Latifa ameyaeleza hayo katika kikao hicho kilichofanyika kati ya Taasisi yake na ujumbe kutoka ubalozi wa China kikiwa na malengo ya kushirikiana katika sekta ya Biashara hususan katika kuboresha mifumo mbalimbali ya biashara.
Kwa upande wake ndugu Lı Jıalu kutoka China ameeleza kuwa watahakikisha wanaiunganisha TanTrade na Taasisi zinazosimamia biashara nchini China ili kuweza kujengeana uwezo katika Nyanja mbalimbali za Teknolojia na biashara