Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE NA TCCIA WAPOKEA UJUMBE (DELEGATION) KUTOKA NCHINI BELARUS

  • January 25, 2024

23 Januari, 2024.

Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ikiongozwa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara, Bw. Fortunatus Mhambe na Afisa kutoka Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Bi. Fatuma Hamis wamekutana na Ujumbe (Delegation) kutoka nchini Belarus uliopo nchini kwa lengo la kukutana na wafanyabiashara, wazalishaji na wanunuzi wa vifaa katika Sekta ya Umeme.

Kupitia kikao hicho, Ujumbe huo uliiomba TanTrade kuwakutanisha na wafanyabiashara wa vifaa vya umeme ili kuzungumza na kubadilishana mawazo ya kibiashara na kujenga mahusiano ya kibiashara baina ya pande hizo mbili.

Vilevile, Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara (DTP) alitumia fursa hiyo kuwakaribisha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar  es Salaam (48 DITF), Maonesho ya Kimataifa ya Wazalishaji (TIMEXPO) na Maonesho ya Madini ya Geita.

Aidha kiongozi wa msafara wa Ujumbe huo Bi Tatiana Sitnikova  alitumia fursa hiyo kushukuru kwa ukaribisho na ufafanuzi waliopewa kuhusu TanTrade na shughuli zake. Vilevile, aliahidi ushiriki wao katika Maonesho ya 48 ya DITF 2024 na kutumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania kushiriki katika Maonesho yao ya Sekta ya Vifaa na Magari ya Kilimo yajulikanayo kama BELAGO yanayofanyika kila mwezi Juni nchini Belarus.