Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE NA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA WAJIPANGA KWA MAONESHO YAKIMATAIFA YA 49 BIASHARA.

  • October 24, 2024

23, Oktoba 2024.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)na Shirika la Posta Tanzania, wamekutana kupanga mpango kazi kwa maonesho yajayo ya 49 ya Biashara maarufu kama (Sabasaba), wakati walipotembelea ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa  TanTrade leo tarehe 23  Oktoba, 2024  zilizopi Kiwanja cha JK Nyerere (Sabasaba) barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), huratibu  maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kila mwaka,  ambayo huwakutanisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, pamoja na taasisi mbalimbali za Umma na binafsi .