Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE NA MABALOZI WA TANZANIA NCHI ZIPATAZO 10 WAJIPANGA KULETA FURSA ZA MASOKO NYUMBANI DAR ES SALAAM

  • September 27, 2023

26 SEPTEMBA, 2023.


Mamlaka ya Maendeleo na Biashara Tanzania (TanTrade) ya kukutana na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali kama vile; Burundi, Qatar, Kenya, Rwanda, China, Misri, Saudia na Algeria katika  ukumbi uliopo ndani ya ofisi  ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade- Dar es Salaam tarehe 26 Septemba, 2023.


Ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara Tanzania (TanTrade) Bi.Latifah M. Khamis ameweza kutoa maelezo juu ya takwimu na mpango mkakati wa taasisi na pia, Mabalozi hao walipata wasaa wa kusema  changamoto zinazowakumba  katika uagizaji na usafirishaji wa mazao na kutoa maoni kuhusu biashara kwa ujumla kwa lengo la kudumisha ushirikiano na kupata fursa mbalimbali ndani na nje ya nchi.