TANTRADE NA IRAN ZAJIZATITI KUPANUA WIGO WA BIASHARA
- September 17, 2025
16, Sept 2025.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade imeketi na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Iran kwa lengo na kuainisha fursa na biashara baina nchi hizo mbili kwenye sekta mbalimbali Kama vile Madini, Petroli, Umeme, Gesi, Madawa ya Binaadamu, pamba za kitabibu, teknolojia, Dhahabu, Kopa, nayobium, manganize, coal, iron mawasiliano nk. Aidha TanTrade kwa umakini Mkubwa imetumia Jukwaa hilo kuzikaribisha taasisi mbalimbali za umma na binafsi kwa lengo la kuwakutanisha na wadau wa Biashara kutoka Iran kwa maslahi mapana ya Umma pamoja na kudumisha ushirikiano wa taasisi za umma na binafsi katika kutekeleza dira ya taifa ya Maendeleo ya 2050.
Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam.