TANTRADE NA BASATA ZAJIPANGA KUTANGAZA UTAMADUNI KATIKA EXPO 2025, OSAKA JAPANI
- February 25, 2025

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imempokea Dkt. Kedmond E. Mapana Katibu Mtendaji wa BASATA akiwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti, leo tarehe 25, Februari 2025, na kutathimini kwa pamoja mchakato wa maandalizi kuelekea Maonesho ya Dunia ya EXPO 2025 Osaka , ambapo Tanzania itashiriki kupitia Taasisi za Umma na binafsi huku sekta mbalimbali kama vile, Biashara, Utalii, Kilimo, Madini, Elimu, Umeme na Usafirishaji zikiwa sehemu ya maonesho haya. Expo 2025 Osaka Japan itaanza tarehe 13 Aprili mpaka 13 Oktoba 2025, Osaka, Kansai Japani.