Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAONGEZA UTAALAMU WA UANDAAJI NA UENDESHAJI WA MIRADI KATIKA NCHI ZINAZO ENDELEA

  • May 27, 2024

25/05/2024
 Tianjin-China
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) siku ya leo imeshiriki mafunzo ya Ujenzi na usimamizi wa Majukwaa huru (Construction and Management of Open Platforms) katika nchi zinazoendelea mafunzo ambayo yamefadhiliwa na Serikali ya watu wa China.

Kupitia mafunzo hayo maafisa wa TanTrade wameweza kupata elimu ya Free Trade Zone ambayo inalengo la kurahisisha na kuvutia uwekezaji wa viwanda ambapo itarahisisha mauzo ya bidhaa  nje ya nchi.

Aidha washiriki wameongeza uelewa kuhusu usimamizi wa ufanisi wa one stop center ambapo katika huduma hii muwekezaji anapata fursa ya kupata sajili mbalimbali katika sehemu mmoja ikiwa ni moja ya mpango wa kurahisha uwekezaji wa viwanda.

Aidha ilipatikana pia  elimu ya maswalaa mengine ikiwemo Free Trade Zones, Development Zones, Special Customs Supervision Zones, High-Tech Development Zones, International Industrial Cooperation Parks & Overseas Economic Cooperation Parks.