Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Michezo kwa Afya..! Tantrade mfano wa kuigwa

  • September 17, 2024

Dar es Salaam

Watumishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), wameshiriki bonanza lilihusisha michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mchezo wa karata, kuvuta kamba, kukimbiza kuku ,Ikiwa ni sehemu ya kujenga afya sambamba na kupata burudani baada ya saa za Kazi.


Aidha katika mchezo wa mpira wa miguu, kabumbu ilipigwa baina ya Kurugenzi ya Usimamizi wa Biashara (DTM) na Kurugenzi ya Ukuzaji Biashara (DTP), ambapo timu zote mbili zilitoa sare ya magoli mawili,  mtanange huo uliopigwa katika Viwanja vya Mwl. Nyerere (Sabasaba) leo tarehe 13, Septemba 2024.