BONAZA LA MICHEZO TANTRADE LAFANA
- September 19, 2025

18 Septemba, 2025.
Katika kuendeleza mshikamano kazini na kuimarisha afya kwa watumishi, TanTrade imecheza michezo ya kirafiki kati ya Utawala na Estate ambapo timu ya utawala kwa upande wa mpira wa miguu imeibuka mshindi dhidi ya Timu ya Estate kwenye michezo ya kirafiki iliyochezwa leo.
Mpira wa miguu Utawala 2 – 0 Estate
Kuvuta Kamba Sare 1 – 1 huku Netiboli Utawala 4 – 3 Estate
Michezo hii imelenga kuhamasisha ushirikiano kazini kuimarisha afya ya mwili na akili ,pamoja na kuongeza morali ya kazi miongoni mwa watumishi wa TanTrade