MAONESHO YA PILI YA WAZALISHAJI YAFUNGULIWA, NEEMA KWA WAFANYA BIASHARA
- September 26, 2024
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Doto M. Biteko ameeleza kuwa Maonesho ya wazalishaji Tanzania (TIMEXPO) ni nyezo muhimu ya kwa wazalishaji wa bidhaa nchini kwa kuwa ni jukwaa la kubadilisha uzoefu na teknolojia mbalimbali ili kuwezesha bidhaa za nchini kupata Masoko ya ndani na nje ya nchi wakati akiyafungua maonesho hayo leo tarehe 26 Septemba, 2024 katika ukumbi wa Ali Hassan Mwinji uliopo katika Kiwanja cha JK Nyerere (Sabasaba) kilichopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Aidha Mhe Dtk Biteko ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) kwa kuandaa maonesho hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa maonesho haya yanakua zaidi .
Vilevile Mhe Dkt Biteko ametoa wito kwa Taasisi wezeshi kuhakikisha zinashiriki ili kuweza kutoa huduma kwa wafanyabiashara nchini.