Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MAONESHO YA PILI YA KIMATAIFA YA VIWANDA YAPAMBA MOTO

  • September 26, 2024

26, SEPTEMBA 2024
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exhaud kigahe(Mb) akiweka sahihi katika kitabu maalum cha wageni baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), ikiwa siku ya kwanza ya ufunguzi ya Maonesho ya pili ya Kimataifa ya Viwanda TIMEXPO.

Aidha maonesho haya yameandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)kwa kuushirikiana  na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) yakilenga kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Viwanda, Wajasiriliamali, wanunuzi ili kupanua wigo na mtandao wa kibiashara ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, Maonesho haya yanafunguliwa rasmi leo tarehe 26 Septemba, 2024, katika kiwanja cha Mwl. JK Nyerere, maarufu kama Sabasaba vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.