MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA FAHARI YA TANZANIA.
- June 26, 2025

26 JUNI 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila aipongenza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kuandaa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba kwa viwango vya Kimataifa ni jambo lakujivunia kwa maendeleo ya biashara na uchumi kwa ujumla. Chalamila amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade kwa kuweka mazingira rafiki ya biashara, kuchagiza matumizi ya nishati safi kwa lengo la kutunza mazingira.
Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa Watanzania wote kutumia fursa za Maonesho ya Sabasaba 2025 kikamilifu, ameyasema hayo katika ufunguzi wa semina ya Washiriki Sabasaba 2025. Leo katika ukumbi wa Rashid Mfaume uliopo Sabasaba Grounds Jijini Dar es Salaam.