SABASABA KUNA KILA KITU, NJOONI SABASABA 2025.
- July 10, 2025

10 JULAI, 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis anaendelea kuwakaribisha Watanzania na wafanyabiashara kutumia vyema jukwa la Maonesho ya Sabasaba kwani lina fursa nyingi kwa maendeleo endelevu ya uchumi. Sabasaba inawakutanisha Watanzania na huduma zote za kijamanii, bidhaa na huduma, kuna kurudani Sabasaba kupitia Kijiji Cha Sanaa, Michezo mbalimbali ya Watoto na Wanyama, ameainisha hayo kwenye mahojiano na kituo cha Habari cha Clouds Fm, kilichoweka makazi yake ndani ya Uwanja wa Maonesho ya Sabasaba 2025. Maonesho ya Sabasaba yameanza tarehe 28 Juni na kutamatika Julai 13, 2025. Sabasaba 2025 "Kidigitali zaidi".