Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

SABASABA KUWEZESHA UBUNIFU, UKUAJI NA KUJENGA UHUSIANO WA KIMATAIFA

  • June 14, 2024

14/06/2024

Maonesho ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam ya mwaka 2024 kuwa chachu ya ubunifu, ukuaji na kujenga uhusiano wa  kimataifa wa kibiashara  kwa wafanyabiashara nchini.


Hayo yametabainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade)  Bi Latifa Khamis wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Dunia nzima iko Temeke “Tukutane 77’’ inayolenga kuihabarisha dunia juu ya matukio mbalimbali yatakayoendelea wakati wa maonesho yatakayoanza tarehe 28 Juni hadi tarehe 13 Julai 2024 alipokua akizungumza katika  kipindi cha Joto la asubuhi kilichofanyika leo katika studio za E-Fm jijini Dar es Salaam .


Aidha Bi Latifa ameeleza kuwa Maonesho haya ya Kimataifa yamekua yakiitangaza Tanzania kimataifa ikiwa ni chachu ya  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ambapo kwa mwaka huu zitahudhuria nchi zaidi ya 24 ambazo  tayari zimethibitisha kushiriki,  pamoja na makapuniu 4000  hukuyakichagizwa na teknolojia mbalimbali za hali ya juu zitakazoleta tija katika uzalishaji.

Kwa upande wa E-Fm ameeleza kuwa Dunia nzima itakuwa Temeke kwa dhana ya E-FM kuhabarisha dunia wakati wote wa maonesho ya Kimataifa ya Dar Es Salaam masuala mbalimbali yatakayojiri wakati wa maonesho hayo.