Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

SABASABA 2025 YAJA KITOFAUTI

  • May 14, 2025

13 Mei, 2025.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade, Latifa Khamis, amesema kuwa maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, yatafanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025 katika viwanja vya Julius Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa CBE jijini Dodoma,  Latifa amesema kaulimbiu ya mwaka huu ni: "Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania." Aidha ameeleza kuwa lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kukutana, kubadilishana uzoefu, kutafuta masoko pamoja na kujifunza teknolojia mpya. Aidha, maonesho haya yamekuwa pia sehemu ya kujifunza kwa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini.