SIKU YA RUSSIA SABASABA 2025 YAFUNGUA ZAIDI MILANGO YA BIASHARA.
- July 10, 2025

9 JULAI, 2025.
Siku maalum ya Taifa la Urusi iliyofanyika kama programu mojawapo kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 ambayo yanaratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imekua daraja la kuwaunganisha wafanyabiashara wajasiriamali wa Kitanzania na wale wa Urusi, wakiangazia sekta mbalimbali kama vile Kilimo, Ujenzi, Madawa, Madini na Teknolojia. Aidha wafanyabiashara kutoka pande zote mbili walipata nafasi ya kufanya mikutano ya Biashara kwa Biashara (B2B) kwa lengo la kuongeza mtandao wa Biashara, fursa za masoko na kubadilishana uzoefu, siku hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Rashida Mfaume Kawawa (Dome) uliopo katika kiwanja cha Mwl Julius Nyerere maarufu (SABASABA grounds).