Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

RAIS SAMIA SULUHU ATOA MUALIKO KWA WAFANYABIASHARA UTURUKI KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA MSIMU WA 48

  • April 23, 2024

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea na ziara yake Nchini Uturuki ambapo siku ya leo ameshiriki ufunguzi rasmi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uturuki katika ufunguzi huo Mh. Rais Samia ametoa Mualiko Maalamu kwa wafanyabiashara wa Uturuki kuweza kushiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba.

Mh. Rais amesema maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam ni maonesho makubwa ya kibiashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na huwa ni chanzo cha fursa mbalimbali ikiwemo kuwakutanisha wafanyabiashara na kuwawezesha kubadilishana taarifa na uzoefu, kujua taarifa mpya za masoko na bidhaa Pamoja na kuuza bidhaa mbalimbali