Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

RAIS MWINYI AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SABASABA 2025.

  • July 7, 2025

7 JULAI, 2025.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefungua rasmi Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 na kuipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambayo ndio mratibu wa Maonesho hayo kwa kuyafanya yawe bora  apongeza matumizi ya teknolojia. Rais Mwinyi ameipongeza TanTrade kwa kufanikisha uandaaji wa kakati wa kuboresha uwanja wa Maonesho wa Mwl. Julius Nyerere (Sabasaba Grounds),(master plan)leo katika ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Sabasaba 2025. Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.