Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MAANDALIZI YA MAONESHO YA 49 YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA DAR ES SALAAM (SABASABA) YASHIKA KASI

  • April 22, 2025

22, Aprili 2025.
Dar es salaam.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  imekutana na Wajumbe wakamati ya Ulinzi na Usalama na kuangazia maswala ya usalama wa Watembeleaji, Washiriki na Mali zao katika kipindi cha maandalizi na wakati wa maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (49TH DITF) 2025 yatakayofanyika kuanzia tarehe 28, Juni  na kutamatika 13, Julai 2025.

Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama kwa kutambua ukubwa wa Maonesho hayo ya Kimataifa ambayo hupokea washiriki wa kigeni kutoka nchi mbalimbali duniani, imeanza mapema maandalizi hayo ili kuhakikisha swala la Ulinzi na Usalama linaimarishwa kwa asilimia mia, katika mkutano uliofanyika leo Jumanne kwenye Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.