Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MAANDALIZI YAMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 85.

  • June 24, 2025

23 JUNI, 2025.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Bi. Latifa M. Khamis ameongea na Waandishi wa Habari nakuainisha ya kwamba maandalizi ya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 yamekamilika kwa asilimia 85, ubora wa Maonesho ya Kimataifa umezingatiwa kwa viwango vya Maonesho ya Kimataifa. Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade ameweka bayana kuwa, ushiriki wa nchi na mikoa mbalimbali umeongezeka jambo litakalopelekea kufana zaidi kwa Maonesho ya mwaka huu Sabasaba 2025, huku programu mbalimbali zikifanyika ndani ya siku mbalimbali wakati wa Maonesho, amesema hayo leo katika ziara ya Mkuu wa Wilaya, katika Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam