FURSA KWA WAFANYABIASHARA UZINDUZI WA SGR, DAR - DODOMA
- August 1, 2024
1 Agosti 2024
Dar es Salaam.
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan leo amezindua rasmi usafiri wa treni ya kisasa (SGR) na kusema kwamba kuanza safari hizi kutasaidia katika kukuza uchumi na kuimarisha Biashara ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Mhe. Rais Aliendelea kusema kwamba Serikali imejikita katika kuhakikisha kwamba Biashara kupitia Soko Huru la Bara la Afrika (AfCFTA) inafanyika kwa wingi zaidi na kuleta mchango chanya katika pato la Taifa kwasababu dhumuni ni kuhakikisha Reli hii inafika mpakani mwa Tanzania na nchi jirani.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa M. Khamis na Mkurugenzi Mkuu wa TTB Bwa. Ephraem Mafuru pia wamehudhuria uzinduzi huu kama viongozi wa Sekta ya Biashara na Utalii, Sekta zinazotazamiwa kuwa na mchango mkubwa kwa SGR.