Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

OMANI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA MAONESHO YA BIASHARA OMANI

  • January 31, 2025

30, Januari 2025


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), imekutana na Ujumbe kutoka Omani na kuangazia maswala ya ushirikiano kwenye maonesho ya Eatixoman, yanayotarajiwa kufanyika tarehe 16 na 17 Aprili 2025 nchini Omani, ambapo Tanzania imealikwa kushiriki katika sekta za kilimo na mafuta walipotembelea ofisi za TanTrade leo tarehe 30 Januari, 2025.

Aidha ujumbe huo umeiombaTanTrade kuwakutanisha na wadau muhimu wa biashara wa hapa nchini watakao shiriki kwenye maonesho ya biashara nchini Omani.

Kwa upande wa TanTrade imeukaribisha Ujumbe huo kutoka Omani kuja na kushiriki kwenye maonesho  ya biashara ya kimataifa ya 49 ya Dar es Salaam  maarufu kama (Sabasaba) yanayotarajiwa kuanza tarehe 28, Juni 2025 mpaka tarehe 13, Julai 2025.