Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KAMPUNI ZAIDI YA 31 KUTOKA UTURUKI YAFUATA FURSA ZA KIBIASHARA NCHINI TANZANIA

  • September 21, 2023

DAR ES SALAAM
19.09.2023

Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade) ikishirikiana na Ubalozi wa Turkiye iliandaa mkutani wa wafanyabiashara na zaidi ya makambuni 100 kutoka tanzania yalifanikiwa kuhudhuria na vilevile kampuni zaidi ya 31 kutoka Uturuki ziliweza kuhudhuria katika mkutano huo. kampuni kutoka Uturuki zililenga kutafuta fursa katika sekta  mbalimbali ikiwepo matunda, mbogamboga, bidhaa za misitu, vipuri vya magari pamoja na zana za kilimo.

Aidha Bi Latifa Khamis (Mkurugenzi Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania) ametoa shukrani za dhati kwa Ndugu Mehmet Gulluoglu ambaye ni Balozi wa Uturuki pamoja na msafara mzima wa wafanyabiashara kutoka Uturuki kwa kujumuika na wafanyabiashara wa Tanzania. Hii inaonesha fika ushirikiano na uhusiano mzuri uliopo baina ya Nchi hizi mbili na kupitia mkutano huwo itazidi kuimarisha na kukuza maendeleo ya biashara baina ya nchi hizi mbili.

Bi Latifa aliendelea kwa kusema kuwa kuna fursa nyingi pia bado hazijafikiwa hapa nchini kwetu hususani pamba na mazao mengi ya kilimo na vilevile kuna fursa ya Uchumi wa buluu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha aliendelea kwa kusema kuwa lengo kuu la kuandaa mkutano huo (B2B meeting) ni kukutanisha mauzaji na wanunuzi ( wafanyabiashara) ili kuweza kubadilishana uzoefu na kuzidi kujifunza kwa lengo la kukuza na kuboresha bidhaa zao na vilevile aliwakaribisha wafanyabiashara wote kutembelea TanTrade ilikuweza kupata melezo zaidi katika fursa za biashara zilizopo Nchini.