WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AIPA HEKO TANTRADE
- August 9, 2024

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Selemani Jafo aipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kuendelea kuwaunganisha wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwapa nafasi ya kuonesha bidhaa zao katika maonesho mbalimbali ya biashara ndani na nje ya nchi.
Aidha, amewapongeza wafanyabiashara waliopo katika banda la TanTrade na kuwapa rai kuendelea kuzalisha bidhaa zenye viwango ili waweze kutafutiwa masoko ya uhakika nje ya nchi.
Dkt. Jafo amesema hayo katika viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma alipotembelea mabanda mbalimbali yalipo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shughuli ya Ufungaji wa Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo (Nanenane).